pmbet

KUMEKUCHA: Vijana Nigeria kuandamana, kisa kupanda kwa gharama za maisha

Eric Buyanza

July 26, 2024
Share :

Rais wa Nigeria, Rais Bola Ahmed Tinubu na Jeshi la nchi hiyo limeonya juu ya kufanyika kwa maandamano ya vurugu kama yaliyotokea nchini Kenya, ambayo yamepangwa kufanyika wiki ijayo nchini humo kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha. 

Tinubu amesema katika taarifa kuwa hawaogopi maandamano bali wasiwasi wao ni kuhusu usalama wa raia na uharibifu ambao huenda ukatokea.

Kiongozi huyo ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuwa waangalifu na kuonya juu ya kuigeuza Nigeria kuwa kama Sudan, ambayo ipo kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 15 sasa.

DW imeripoti kuwa maafisa wa serikali, vikosi vya usalama na magavana nchini Nigeria wamewaomba vijana kujiepusha na maandamano hayo, huku baadhi ya viongozi wakiwashutumu waandaaji wa maandamano hayo kwa uhaini na kuwa na nia ya kuliyumbisha taifa.

Kumetolewa miito katika mitandao ya kijamii kwa Wanaigeria kufanya maandamano kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha kuanzia Agosti mosi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet