"Kuna kitu sijakielewa kwenye uchezaji wa Nathananiel Chilambo" Mkeyenge.
Joyce Shedrack
August 28, 2026
Share :
"Ananivutia mchezaji mpya wa Simba anayeitwa Nathaniel Raphael Chilambo. Kijana anaonekana ana tank kubwa lililojaa mafuta. Anakimbia kilomita nyingi kiwanjani bila kuchoka.
"Lakini kuna kitu sijakielewa katika game yake. Sijui ni mwalimu Steven Barker anamtuma afanye anavyofanya kiwanjani au ni utashi wake binafsi.
"Chilambo ni mlinzi wa pembeni. Anacheza kulia. Anacheza kushoto, tena kwa ustadi na ubora mkubwa. Ana balance nzuri. Katika mechi nyingi nilizomuona ndani ya jezi ya Simba, akipangwa pembeni huwa anaingia hadi kati, muda mwingine anasogea juu kabisa kama mshambuliaji wa mwisho.
"Nilimuona hivi kuanzia kule Rwanda. Nikamuona hivi katika tamasha la Simba Day. Katika michezo ya Ligi kwenye mechi alizocheza alicheza hivi hivi. Binafsi imeanza kunitisha.
"Mtaani wachezaji kama hawa tunawaita ‘Chaboli’. Kila unapodunda mpira nae yupo. Hii ni nzuri mkikutana na timu ambayo muda mwingi inakaa chini kuwasubiri mje ndio wao ‘wareact’.
“Lakini siku mkikutana na timu ambayo na yenyewe ina quality kubwa na haina muda wa kukaa nyuma kuwasubiri hapo ni majanga kwa mchezaji na majanga kwa timu”.Ameandika Mkeyenge.





