pmbet

Kuna wakati Como walikuwa kama wapo 12 uwanjani - Ferdinand

Eric Buyanza

October 22, 2026
Share :

Beki wa zamani na nguli wa Manchester United, Rio Ferdinand, amewatolea uvivu wachezaji wa klabu hiyo kufuatia kipigo cha aibu cha 4-1 kutoka kwa klabu ya Italia ya Como kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) usiku wa kuamkia Alhamisi.

 

Ferdinand, ambaye alikuwa akifuatilia mechi hiyo iliyopigwa nchini Italia, alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) kueleza hasira na masikitiko yake makubwa, akidai kuwa timu hiyo kwa sasa haina makali kabisa na haina morali wa kupambana.

 

Katika ujumbe wake huo uliosambaa kwa kasi, Ferdinand alisema kikosi hicho chini ya kocha Michael Carrick kilionekana kuzidiwa kete kwenye kila idara uwanjani na vijana wa kocha Cesc Fàbregas.

 

"Como ya Cesc Fàbregas imetufanya tuonekane kama timu iliyoshinda BAHATI NASIBU ili kuingia Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kuna nyakati ilionekana kana kwamba Como walikuwa na wachezaji 12 uwanjani," aliandika Ferdinand.

 

"Tulikuwa hatuna MENO kwenye safu ya ushambuliaji. Hakuna nguvu ya kukimbia kwenye timu. Tulishindwa kabisa kuwakaba Como, na hatukuwa na mwelekeo wowote tukiwa na mpira" alimalizia Ferdinand.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet