pmbet

Kuna wakati unafungwa na huwezi kuelezea - Mourinho

Eric Buyanza

September 5, 2026
Share :

Licha ya kupata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Real Betis usiku wa Ijumaa, Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho, amewapongeza wachezaji wake wawili.

Mourinho alishuhudia Betis ikiifunga Madrid katika Uwanja wa La Cartuja, kupitia bao pekee la mchezo huo lililofungwa na Troy Parrott.

 

Akizungumza katika mahojiano ya baada ya mchezo, Mourinho aliwapongeza mabeki wa kati Ibrahima Konate na Dean Huijsen kwa kumudu vyema mchezo huo, akiongeza kuwa walionyesha kiwango cha hali ya juu.

 

"Timu ilicheza mchezo mzuri. Wakati mwingine unapoteza na hujui sababu au jinsi ya kulielezea hilo," alisema Mourinho.

“Tulitawala mchezo kwa kiasi kikubwa; mabeki wa kati walionyesha kiwango cha hali ya juu na kudhibiti kila kitu. Kulikuwa na mashambulizi mengi na nafasi nyingi za kufunga mabao.”

 

Sasa Real Madrid itakutana na Inter Milan katika Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet