Kundi la Hezbollah laishambulia Israel, wadai ni kulipa kisasi!
Eric Buyanza
January 9, 2024
Share :
Kundi la Hezbollah nchini Lebanon,limesema leo kwamba limefanya shambulizi la droni dhidi ya kituo cha kamandi ya jeshi la Israel kama sehemu ya kujibu mauaji ya kiongozi wake mwandamizi Wissam Tawil yaliyofanywa jana Jumatatu na mauaji ya wiki iliyopita ya naibu mkuu wa kundi la Hamas.
Kundi hilo limefahamisha kwamba limeshambulia katika makao makuu ya jeshi kwenye eneo la Safed ikiwa ni mara ya kwanza kuwahi kulilenga eneo hilo.