Kunipata kwa 'Show' jipange na Milioni 5
Eric Buyanza
January 2, 2024
Share :
Mkali wa Amapiano, Chino Kid baada ya kufunga mwaka vizuri amefunguka kuwa ili kumpata kwa ajili ya kuburudisha wapenzi wa muziki unatakiwa kuandaa bajeti ya Milioni 5.
Mkali huyo ambaye amekuwa bora kwenye kuimba na kucheza anasema…“Nilianza kwa kuwa dansa nikitumika na msanii Marioo, lakini sasa nimesimama kuimba na kucheza, nafurahi nimekuwa bora sekta zote mbili.....Mwaka 2023, umekuwa wa mafanikio makubwa kwangu nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa kujiweka kwenye ushindani, ukitaka kunipata niburudishe mashabiki kwa ‘show’ unatakiwa kuwa na kitita cha milioni 5 na inategemea na sehemu ninayopelekwa.” anasema.
Chino Kidd, anaweka wazi kuwa mwaka 2023 aliongia kwenye muziki kama muimbaji, ni mwaka ambao jina lake limekuwa tofauti na miaka aliyodumu kwenye sanaa hiyo akiwa mnenguaji.
NMG