Kunyonya vidole kunaharibu muonekano wa sura yako
Eric Buyanza
March 6, 2024
Share :
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Kinywa na Meno katika Wizara ya Afya, Dk. Baraka Nzobo, ameitaja tabia kunyonya vidole hasa gumba, kwa baadhi ya watu wazima na watoto kuwa moja ya tabia inayosababisha uduni wa afya ya kinywa na meno.
“Tabia hii huanza toka toka utotoni na baadhi ya watoto wanashindwa kuiacha na kuendelea kunyonya dole gumba hadi wakiwa watu wazima. Tabia hii ya kunyonya dole gumba husababisha meno ya mbele ya taya la juu na chini kushindwa kukutana mtu anapofunga mdomo."
“Ukimwambia ng’ata meno, basi meno ya nyuma yatakutana, lakini meno ya mbele kamwe hayawezi kuKUtana. Hii husababisha kuharibu muonekano mzuri wa sura ya mtu huyo."
“Mzazi ambaye ana mtoto ananyonya dole gumba na ameshindwa kuacha tunamshauri ampeleke kwa Daktari wa Kinywa na Meno atamsaidia mtoto huyo kumpatia tiba ya kuacha kunyonya dole gumba,” amesema.
NIPASHE