pmbet

"Kuongezeka Home Studios kunaathiri Muziki" - Roma

Sisti Herman

March 19, 2024
Share :

Ikiwa ni siku chache tangui msanii Diamond Platnumz aonyeshe muonekano wa kisasa wa studio yake binafsi ya nyumbani ya kurekodia nyimbo, msanii wa Hip-hop nchini Roma Mkatoliki amesema kupitia kurasa zake za kijamii ambazo huwa anazitumia mara kwa mara kutoa mawazo na maoni yake amesema kuwa kuongezeka kwa studio binafsi kunapunguza kwa kasi ubunifu, ushirikiano na ubora wa kazi za wasanii.

 

Hizi ni nukuu za Roma

 

 "Ongezeko la Home Za Wasanii Wetu Lina Faida✅ But Kwa Namna Fulani Lina Athiri Tasnia Kwa Kushindwa Kupata Nyimbo BORA Nyingi Now Days!! Iko Hiviii, Zamani Studio Zilikuwa Chache, Na Wasanii Hawakuwa Na Studio Majumbani Kwao, Hivyo Ililazimu Ukitaka Kufanya Beat Au Kurekodi Ngoma Ni Ufunge Safari Kuifata Studio Ilipo!"

 

“Hii Ilisaidia Sana Wasanii Kukutana Na Kuonana Mara Kwa Mara Na Kusaidiana Ideas Kutengeneza Wimbo Bora, Pia Ilifanya Kuwe Na Colabos Nyingi Sana Za Wasanii Tofauti Tofauti!! Lakini Kubwa Ni Ile MindSet, Kitendo Cha Kusafiri Mwanza To Dar Kuja Kurekodi Au Kuchukua Tu Beat, Au Kutembea Kimara To Masaki Aaf Urudi Home Ukajifue”

 

“Hii Ilitupa Hasira Ya Kufanya Kitu Bora, Plus Mistari Ushaimeza Sana Na Umeizoea Beat Siku Ya Vocal Lazima Uue!! NowDays Studio Ziko Home, Unapata Idea Ya Ngoma Usiku Unaamka Apo Apo Unamuita Producer Unarekodi, Wengine Wanajirekodi Wenyewe!! Hata Hupati Muda Wa Kuandika, Kuizoea Beat/Flow/Melody Yani Unachapa Tu, Mixing Fasta Una Export Mzigo Unarease Asubuhi!!”

 

Yapi maoni yako kuhusu hili kwenye kiwanda cha burudani?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet