pmbet

Kupanda bei ya mafuta, mawaziri marufuku kusafiri nje

Eric Buyanza

April 4, 2026
Share :

Serikali ya Senegal imepiga marufuku mawaziri wake kufanya safari za nje ya nchi zisizo za lazima kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta duniani kunakosababishwa na mzozo wa Iran, waziri mkuu ametangaza.
 

Akizungumza jana Ijumaa, Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko alisema kuwa gharama ya sasa ya pipa la mafuta inakaribia kuwa mara mbili ya kiwango kilichokuwa kimepangwa kwenye bajeti.

 

Sonko ameahirisha pia safari zake binafsi kwenda Niger na Hispania kama sehemu ya hatua hizo za kubana matumizi.

Aliongeza kuwa waziri wa madini atatangaza hatua zaidi za kupunguza matumizi ya serikali katika wiki ijayo.

 

Hatua ya Senegal ni miongoni mwa hatua za hivi karibuni barani Afrika dhidi ya kupanda kwa bei ya mafuta, hali ambayo imesababisha baadhi ya nchi kupunguza tozo za mafuta na kuweka mgao wa umeme.
 

Katika hotuba yake kwa vijana, waziri mkuu alisema hataki kuwatisha wala kuwawekea shinikizo, bali anataka kuwapa uelewa kuhusu hali halisi ya dunia ilivyo ngumu kwa sasa.
 

Hata hivyo, alisisitiza kuwa licha ya changamoto, wananchi wa Senegal wameendelea kuwa na ustahimilivu mkubwa.

 

Licha ya kuwa na sekta changa ya mafuta na gesi, Senegal bado inategemea kwa kiasi kikubwa uagizaji wa mafuta kutoka nje.

 

Mwaka uliopita, IMF iliielezea uchumi wa Senegal kuwa imara, ikiwa na ukuaji wa karibu asilimia 8 na mfumuko mdogo wa bei.

 

BBC

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet