'Kupitia mimi Singeli inaenda kutambulika kimataifa - Dvoice
Eric Buyanza
December 22, 2023
Share :
Msanii wa singeli kutoka WCB Wasafi, Dvoice Ginni maarufu D Voice amesema bado anajitafuta ili afikie anga za kimataifa kama walivyo wasanii wengine wa kundi hilo.
D Voice anayefanya vizuri na ngoma kama ‘Kuachana Shingapi’ na ‘Madanga ya Mke Wangu’ amesema...
“Wasanii wengi wakiona wanakubalika baadhi ya mitaa wanaamini wamemaliza wanaridhika, mimi naona bado najitafuta kuelekea mafanikio ya kufanya shoo kubwa za kimataifa kama wanavyofanya wasanii wengine kama Mboso na bosi wangu Diamond,” amesema D Voice.
D Voice amesema kuwa WCB itasaidia kunyanyua muziki wa singeli huku akiamini kwamba muziki wa singeli unakwenda kupata heshima kubwa.
“Naamini mimi kuwa WCB kutabadilisha fikra ya muziki wa singeli, kupitia mimi unakwenda kututambulisha kimataifa na mafanikio pia,” amesema D Voice.