pmbet

Kupona saratani hadi fainali Afcon, safari ya maajabu ya Haller

Sisti Herman

February 8, 2024
Share :

Nyota wa timu ya Taifa ya Ivory Coast Sebastian Haller ambaye jana alifunga goli lililowapa ushindi jana dhidi DR Congo kwenye nusu fainali ya kombe la mataifa Afrika (AFCON 2023) anaweza kuwa ndiye mchezaji mwenye bahati na historia ngumu na kipekee kati ya wachezaji wote waliocheza Afcon msimu huu wa 33 kutokana na misukosuko ya kiafya aliyopitia ndani ya miaka miwili iliyopita.

 

Mchezaji huyo mzaliwa wa Ufaransa, mwaka 2022 aligundilika kuwa na saratani ya tezi dume ambayo alipambana nayo kwa karibu mwaka mzima kwa matibabu ya namna tofauti na baadaye mwezi februari mwaka 2023 alishinda vita hiyo na kurejea uwanjani kunako klabu ya Borrussia Dortmund ya ligi kuu nchini Ujerumani.

 

Haller jana alifunga bao lililowaondoa DR Congo kusaka taji lao la 3 na Ivory Coast sasa wanamenyana na Nigeria katika pambano linaloweza kuwa la kufana katika Uwanja wa Alassane Ouattara Jumapili jioni.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet