pmbet

Kurejea kwa Cosmas Cheka, kutikisa jiji Oktoba 31

Eric Buyanza

October 21, 2026
Share :

Mashabiki wa masumbwi nchini wanatarajia kushuhudia usiku wa kihistoria wa burudani hiyo inayotarajiwa kutikisa jiji la Dar es Salaam Oktoba 31, 2026.

 

Baada ya kukaa nje ya ulingo kwa kipindi kirefu, bondia mwenye uzoefu mkubwa na aliyewahi kutwaa ubingwa wa WBO Asia Pacific, Cosmas Cheka, atashuka ulingoni kulinda heshima yake dhidi ya bondia Omary Sultan kwenye pambano la raundi nane la uzani wa Super Middleweight.

 

Usiku wa pambano hilo uliopewa jina la "The Night to Remember" unatarajiwa kuwa kivutio kikubwa na utafanyika katika ukumbi wa The Sky Wave, uliopo Msasani Beach.

 

Akizungumza kuelekea pambano hilo, Cheka amebainisha kuwa kurudi kwake ulingoni si kwa ajili ya kuongeza idadi ya rekodi tu, bali ni nafasi ya kuthibitisha ubora na uzoefu wake baada ya kuwa nje ya ulingo kwa muda mrefu.

Usiku huo umeandaliwa na Fayheroes Sports Promotions.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet