Kusaga atembelea familia ya Gardner, amwaga machozi
Sisti Herman
April 28, 2024
Share :
Ikiwa ni siku chache tu tangu tasnia ya habari impoteze nguli Gardner G Habash, leo Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amefika katika kijiji cha Kikelelwa, Tarakea Wilayani Rombo nyumbani kwa aliyekuwa Mtangazaji huyo kutoa pole kwa Baba Mzazi wa Gardner pamoja na familia kwa ujumla kufuatia msiba huo mkubwa.
Mkurugenzi Kusaga amemueleza Mzee Gabriel Habash namna gani ameguswa na msiba huo kutokana na ukaribu wake na Captain G. ambaye pengo lake kwa Clouds Media na Tasnia ya habari halitozibika na kusikitika kushindwa kuhudhuria mazishi kutokana na kuwa nje ya Nchi.