Kusoma magazeti kwa mbwembwe ni ubunifu - Nape
Eric Buyanza
February 15, 2024
Share :
Waziri wa Habari na Mawasiliano, Mhe. Nape Nnauye, ameielekeza Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, kuruhusu ubunifu kwenye tasnia ya Habari.
Maelekezo hayo yamefuata siku moja baada ya Mamlaka hiyo kuzuia usomaji wa magazeti kwa mbembwe, ambapo amebainisha kuwa staili mbalimbali za usomaji magazeti zimeongeza mvuto kwenye usomaji wa magazeti, hivyo jambo hilo ni la kutiwa moyo na sio kuzuiliwa.
Mhe. @napennauye ametoa maelekezo hayo kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), ambapo pia ameitaka Mamlaka hiyo, kujenga utamaduni wa kuzungumza kabla ya kuagiza.