Kutana na 'Baby Tingzi', mwanamke mwenye kilo 25 anayetaka kukonda zaidi
Eric Buyanza
July 11, 2024
Share :
Mwanamke huyu wa kichina mwenye uzito wa kilo 25 tu, anafahamika zaidi kwa jina la Baby Tingzi na amejipatia umaarufu baada ya kuonyesha mwili wake mwembamba wa kushangaza mtandaoni huku akidai anataka kupungua zaidi ya hapo.
Wengi wa mashabiki zake wamekuwa wakionyesha wasiwasi wao juu ya afya yake lakini mwenyewe hupuuza na kudai anapendelea kuwa mwembamba na kuongeza kuwa muonekano wake huo ambao kwa sehemu kubwa unaonyesha mifupa haumuogopeshi lolote.