pmbet

Kutana na binadamu mwenye ngozi inayovutika zaidi duniani

Sisti Herman

February 21, 2024
Share :

Gary Turner ambaye ni raia wa Uingereza anashikilia rekodi ya dunia ya Guinness kuwa binadamu mwenye ngozi inayovutika zaidi duniani.

Turner mwenye umri wa miaka 56 aliweka rekodi hiyo baada ya kufanikiwa kuivuta ngozi yake kwa inchi 6.25 mwaka 1999, nchini Marekani katika mji wa Los Angles.

Kupitia uwezo wake huu alifanikiwa kuigiza kwenye movie iitwayo ‘He Took His Skin Off For Me’ na amekuwa akijiingizia kipato kupitia matamasha mbalimbali ya kuonesha uwezo wake huo.

Turner aliwahi kuwa kwenye ndoa na mwanamke aliyefahamika kwa jina la Carli Norris mwaka 2005 na walipeana talaka mwaka 2014.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet