pmbet

Kutana na Sanjoy Rabidas, shujaa wa kweli wa maisha!

Eric Buyanza

March 21, 2026
Share :

Ingawa watoto wengi wa rika lake hufurahia maisha kwa kutegemea wazazi, Sanjoy alitumia saa masaa 12 kwa siku kung'arisha viatu vya wateja wake, na kisha akikesha mpaka usiku wa manane akijisomea chini ya mwanga hafifu wa kibatari. Umaskini ulijaribu kumvunja moyo, lakini ujasiri wake, hamasa na njaa ya maarifa ilimfanya aendelee.
 

UNAJUA NINI KILITOKEA?

Aliongoza shule yake kwa kupata alama 465/500 (93%) katika mitihani yake ya Bodi ya Bengal Magharibi huko nchini India!

 

Akiwa na ndoto kubwa, Sanjoy anatamani kuwa Ofisa wa Polisi, akithibitisha kwamba hakuna mapambano yenye nguvu zaidi ya nia ya kufanikiwa.

 

Huenda asiwe na utajiri, lakini amebeba kitu chenye thamani zaidi - tumaini lisilotikisika, bidii, na uthabiti.
 

Shujaa huyu hajasafisha viatu tu, lakini pia alisafisha hatima yake!

Endelea kuamini, endelea kufanya kazi, na mafanikio yatakufuata!

Mafanikio hayahusu rasilimali, ni kuwa mbunifu!

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet