Kutana na Simba, mbuzi mwenye masikio yaliyopitiliza!
Eric Buyanza
December 29, 2023
Share :
Mbuzi mdogo mwenye masikio marefu anayejulikana kwa jina la Simba amekuwa gumzo kunako vyombo vya habari nchini Pakistani.
Mfugaji wa Simba, Mohammad Hassan Narejo, anasema ndani ya siku 10 hadi 12 baada ya kuzaliwa kwake tayari alikuwa anaonekana kwenye vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa.
Kwa mujibu Narejo ndani ya siku 30 tu baada ya kuzaliwa kwake alipata umaarufu mkubwa mno jambo ambalo lingeweza kumchukua binadamu wa kawaida hata miaka 25 hadi 30 kufikia kiwango cha umaarufu wa mbuzi huyo.
Masikio ya Simba ni marefu kiasi kwamba Narejo analazimika kuyakunja mgongoni ili kumzuia asiyakanyage.