pmbet

Kutoka kusugua benchi Dortmund hadi kuwa dhahabu Barcelona!

Eric Buyanza

September 19, 2026
Share :

Katika ulimwengu wa soka, mambo hubadilika kwa kasi ya ajabu, lakini hadithi ya Karim Adeyemi katika mwaka wa 2026 imeacha wengi vinywa wazi. Ndani ya miezi michache tu, nyota huyu wa kimataifa wa Ujerumani ametoka kwenye kipindi kigumu cha kusugua benchi hadi kuwa mmoja wa wachezaji hatari na wanaozungumziwa zaidi barani Ulaya.
 

Mapema mwaka huu, ukweli wa maisha ya Adeyemi ulikuwa wa kusikitisha. Akiwa na klabu ya Borussia Dortmund, alipoteza namba katika kikosi cha kwanza na kujikuta akitokea benchi mara kwa mara. Kukosekana kwa mwendelezo wa kiwango bora na majeraha ya hapa na pale vilimfanya akose ujasiri.

 

Pigo kubwa zaidi lilikuja pale alipoachwa nje ya kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kilichoshiriki Kombe la Dunia la 2026. Kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 24 na kipaji kikubwa kama chake, hiyo ilikuwa ishara kwamba taaluma yake ilikuwa ikirudi nyuma.
 

Kila kitu kilibadilika msimu wa kiangazi wa 2026. FC Barcelona, chini ya kocha mkuu Hansi Flick, ilichukua uamuzi uliowashtua wengi kwa kumsajili Adeyemi kwa dau la Euro milioni 22 pekee—dau ambalo kwa sasa linaonekana kama "wizi wa mchana kweupe" kutokana na thamani yake.

 

Flick, ambaye alikuwa kocha aliyempa Adeyemi nafasi ya kwanza kabisa kwenye timu ya taifa miaka ya nyuma, alijua namna ya kutumia kasi yake ya hatari. Tangu atue Catalonia, Adeyemi amekuwa moto wa kuotea mbali:
 

Katika mechi zake saba za kwanza za La Liga na Champions League, tayari ameshafunga mabao 3 na kutoa pasi 3 za mabao (assists).

 

Ingawa alisajiliwa ili kuongeza nguvu ya ziada kikosini, kiwango chake kimemlazimisha Flick kumjumuisha moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza, akishirikiana vyema na Lamine Yamal na Raphinha.
 

Mabadiliko haya makubwa ya kiwango huko Uhispania yalimfanya kocha mpya wa timu ya taifa ya Ujerumani, Jürgen Klopp, ashindwe kumpotezea. Klopp amemwita rasmi Adeyemi kurejea kwenye kikosi cha wazee wa kazi (Die Mannschaft) kwa ajili ya michuano ya Nations League.

 

Hadithi ya Karim Adeyemi inatufundisha nini?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet