pmbet

Kutoka kuwa Rais wa Nchi mpaka kuishi 'banda la uani' na kunywa pombe za kienyeji

Eric Buyanza

May 22, 2024
Share :

Hakika dunia ni mwalimu wa mengi na inatufunza mengi sana ya kushangaza. Wengi hawamjui lakini Valentine Strasser alikuwa rais wa Sierra Leone kati ya Mwaka 1992 mpaka 1996, na aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi kuingia madarakani akiwa na miaka 25.
 

Strasser alichukua madaraka baada ya kumpindua aliyekuwa Rais wa pili wa nchi hiyo Joseph Saidu Momoh ambaye alitorokea Conakry nchini Guinea.

Akiwaongoza vijana wenzake sita walifanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).

Baada ya kuchukua madaraka maisha yakabadilika, hakulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma huku akifuja Almasi ya nchi hiyo.


Kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day akaifanya kuwa sherehe ya kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo.
 

Kiujumla alikuwa mtu wa starehe sana na mpenda wanawake. Strasser aliua watu wasio na hatia na akasahau ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake.

Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada na akakimbilia Uingereza, akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza masomo ya sheria, akasema anataka awe wakili ili awatetee Waafrika.
 

Mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha, akaacha chuo, mwisho akarudi Sierra Leone, akafanya biashara nyingi zikamshinda na kuamua kurudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani. Hata sasa, akiwa na umri wa miaka 49, anakunywa pombe za kienyeji mtaani.
Hana hadhi yoyote kama kiongozi mkuu wa nchi mstaafu. Strasser anaishi kama mtu wa kawaida tu mtaani. Mlevi na hakuna anayemjali.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet