Kuungana tena na Ronaldo? Varane awekewa mezani Pauni milioni 50!
Eric Buyanza
February 7, 2024
Share :
Mabilionea wa kiarabu na wamiliki wa klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia, wanataka kuwa mbele kwenye foleni ya kumfukuzia defender wa Manchester United, Raphael Varane pale atakapokuwa tayari kuondoka.
Klabu hiyo ya mjini Riyadh tayari imemuandalia Varane dau la mkataba wa pauni milioni 50 kwa mwaka ili kumshawishi kuichezea klabu hiyo.
Iwapo Varane atakubali kucheza Al-Nassr, basi ataungana na Ronaldo kwa mara nyingine tena, wawili hao waliwahi kucheza pamoja Real Madrid kwa miaka mitano na walishinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa pamoja.