Kvaratskhelia nje msimu mzima!
Eric Buyanza
October 21, 2026
Share :

Nyota wa Paris Saint-Germain (PSG), Khvicha Kvaratskhelia, anakabiliwa na kipindi kigumu baada ya kuripotiwa kupata jeraha la goti katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona.
Kvaratskhelia aliumia goti la kulia wakati wa mchezo huo uliofanyika Oktoba 20, 2026, ambapo PSG iliibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Barcelona.
Ripoti za awali zinaeleza kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Georgia anadaiwa kupasuka kano ya mbele ya goti (ACL), jeraha linaloweza kumuweka msimu mzima wa 2026/2027.
Mchezaji huyo alilazimika kutolewa uwanjani kabla ya mchezo kumalizika, hali iliyozua wasiwasi kuhusu hali yake na mchango wake katika michezo ijayo ya klabu hiyo.
Jeraha la ACL kwa kawaida huhitaji matibabu ya kina na wakati mwingine upasuaji, huku muda wa kurejea uwanjani ukitegemea ukubwa wa jeraha na maendeleo ya mchezaji katika kipindi cha matibabu.





