Kwa ahadi hii, Je Yanga watotoboa???
Eric Buyanza
December 8, 2023
Share :
Taarifa kutoka mitaa ya Twiga na Jangwani zimethibitisha kuwa Tajiri wa Yanga Ghalib Said Mohamed ‘GSM’ na uongozi wa klabu hiyo umetoa donge nono la shilingi Milioni 100 kwa kila bao litakalopatikana leo kwenye mechi yao dhidi ya Medeama.
Hata hivyo Yanga inafahamu kwamba malengo yao hayo hayataweza kutimia kirahisi kwani Medeama sio timu rahisi ikiwa nyumbani, rekodi zikionyesha kwenye mechi zao tatu za nyuma za ligi ya mabingwa wameshinda zote dhidi ya Remo Stars (1-0),Horoya AC (3-1) na Belouizdad (2-1).