pmbet

Kwa trump, mtoto wa miaka 14 anaruhusiwa kumiliki leseni ya udereva

Eric Buyanza

May 4, 2026
Share :

#JeWajua Katika baadhi ya majimbo nchini Marekani, mtoto wa miaka 14 anaweza kupata leseni ya udereva, ingawa sheria hizi hutofautiana sana kati ya jimbo na jimbo.
 

Sababu kubwa zinazosababisha watoto hao kupata ruhusa ya kumiliki leseni ni mazingira ya kijamii na kiuchumi katika majimbo husika.

 

Kwa mfano katika majimbo kama South Dakota na Kansas, watoto mara nyingi huhitajika kusaidia kazi za shambani ambazo zinahusisha kuendesha mitambo au magari kubebea ya mazao.
 

Pia katika maeneo yenye watu wachache, mabasi ya shule yanaweza yasiwafikie wote, hivyo watoto huruhusiwa kuendesha wenyewe kwenda shule.
 

Pamoja na kupewa leseni hizo lakini bado kuna masharti kadhaa ikiwemo, kutoendesha usiku, marufukuku kubeba abiria na pia kutotumia simu wakati wa kuendesha chombo hicho.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet