Kwaheri Adidas, mipira ya Nike sasa kutumika rasmi mashindano ya UEFA
Eric Buyanza
November 21, 2026
Share :

Nike inatarajiwa kuchukua nafasi ya Adidas kama msambazaji rasmi wa mipira ya mechi kwa ajili ya mashindano ya klabu ya UEFA kuanzia msimu ujao.
Kampuni hiyo kubwa ya Marekani inayotengeneza vifaa vya michezo itabuni mipira itakayotumika katika mashindano mbalimbali ya UEFA, hatua ambayo inahitimisha ushirikiano wa Adidas ulioanza mwaka 2001.
Baada ya zaidi ya miongo miwili, Ligi ya Mabingwa (Champions League) na mashindano mengine ya UEFA sasa yatakuwa na msambazaji mpya wa mipira.





