Kwanini Thomas Muller amempa farasi wake jina la mwanamuziki huyu?
Eric Buyanza
March 23, 2024
Share :
Mshambuliaji wa timu ya Bayern Munich ya Ujerumani, Thomas Muller anajulikana na mashabiki zake kama mtu mcheshi na mwenye vituko ambaye huwa haipita muda bila kufanya kitu cha kuwafurahisha.
Safari hii amekuja na nyingine kuwapa burudani mashabiki zake kwa kupost video akimbusu puani farasi wake mpya aliyempa jina la Kylie Minogue.
Ifahamike Kylie Minogue ni mwanamuziki wa Pop na muigizaji wa Ki-Australia maarufu duniani aliyetamba sana miaka ya mwanzo ya 2000.
Wakati Bayern Munich iliposhinda dhidi ya Darmstadt wiki iliyoisha Muller kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa na furaha alikwenda kumbusu puani na kumpa habari za ushindi farasi huyo...huku akilitambulisha kwa mashabiki jina jipya la farasi kuwa ni Kylie Minogue.
Haijafahamika kwanini Muller ameamua kumpa farasi wake jina la mwanamuziki huyo.