pmbet

"Kwanza Loemba hajaletwa na Jayrutty"Magori.

Joyce Shedrack

April 7, 2026
Share :

Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Crescentius Magori amewajibu waliozusha maneno ya kiungo wao Inno Loemba kutokucheza kisa ni mchezaji aliyesajiliwa na Mzabuni wao wa jezi Jayrutty.

 

“Kwanza Loemba hajaletwa na JayRutty, alitafutwa na Kamati ya Usajili kwa kushirikiana na kocha. Mkataba wa JayRutty ndio unasema atasajili mchezaji mmoja ndio tukamwambia alipie gharama zake za usajili.
Loemba akabidhiwa gari, wengine kufuata - SpotiLEO
"Kwani Mohammed [Dewji] anavyosajili wachezaji kwahiyo ni wachezaji ni wa Mohammed. Na mkataba wa JayRutty unasema kila mwaka atasajili mchezaji mmoja hivyo na mwakani mjiandae kuna mchezaji mwingine atalipia gharama za kumsajili.

"Loemba aliumia tangu mechi ya Singida na alianza mazoezi juzi na kocha akamuweka benchi mechi ya Azam. Hakucheza sababu mwalimu aliona bado timu inayocheza ipo vizuri na hakutaka kuchukua risk ya kumchezesha.”- Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Crescentius Magori.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet