pmbet

Kwenda haja ndogo kabla ya tendo, kutakuepusha na magonjwa

Eric Buyanza

March 12, 2024
Share :

Kitu ambacho kinapaswa kuzingatiwa na jinsia zote mbili (wanawake/wanaume) kwa mujibu wa wataalamu ni kwenda haja ndogo kabla na baada ya kufanya tendo la ndoa. 

Thamara Martínez Farinós, mwanasaikolojia na mtaalamu ya masuala ya ngono katika Taasisi ya Espill anasema.... "Wapenzi kwenda haja ndogo kabla na baada ya kufanya tendo la ndoa ni moja ya njia muhimu ya kujiepusha na magonjwa yanayosababishwa na bakteria.... kunasaidia kusafisha kibofu cha mkojo, hali ambayo inazuia bakteria kuathiri sehemu hiyo." 

Kwa mujibu wa Thamara, tabia hii ukiizoea ni nzuri kwani unaweza kuzuia magonjwa yanayoathiri njia ya kupitisha mkojo kwa kiwango kikubwa. 

Kulingana na mtaalamu huyo, wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya magonjwa yanayoathiri njia ya kupitisha mkojo....hivyo basi inapendekezwa wawe na mazoea ya kwenda haja dakika 15 kabla ya kushiriki tendo la ndoa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet