Kwenye mwezi mmoja, watu wapata 300 wamekatwa miguu
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
Miezi 11 ya vita nchini Sudan imesababisha machungu kwa watoto na vijana ambako ujumbe wa hivi karibuni wa shirika moja la Umoja wa Mataifa uliozuru hospitali kwenye mji mkuu Khartoum umeshuhudiwa vijana waliokatwa miguu, huku Mkurugenzi wa hospitali hiyo akisema mwezi mmoja uliopita pekee watu wapatao 300 walikatwa miguu yao kutokana na madhara ya vita.