Kwenye wimbo 'Naskia Harufu' kwa asilimia 80 huyu unayemuona hakuwa Chidi Benz
Eric Buyanza
January 15, 2024
Share :
Director maarufu wa video za muziki hapa Bongo, Black X ambaye kwasasa anafanya vizuri na video ya wimbo wa msanii Roma Mkatoliki akimshirikisha Chidi Benz (Nasikia harufu), amesema kwenye video ile yule mnayemuona kama Chidi Benz kwa asilimia 80 hakuwa yeye.
Kwa mujibu wa X, wakati wanaanza project ya kushoot wimbo huo Chid Benz alikuwa anaumwa sana hivyo kuna baadhi ya matukio hakuweza kuyafanya na akalazimika kutafuta mtu mwingine wa kuchukua nafasi yake.
"Chidi Benz hakuwa na uwezo wa kufanya movements...ile shot yake ilitaka awe anatamba pale...anaenda anarudi, hakuwa na hiyo capability ya kutembea namna hiyo kwahiyo mule ndani kuna cheating nyingi sana ambazo zimefanyika kufanya ionekana ana move ana power..ndio hivyo nilitafuta mtu akafanya stunt zake."
Alipoulizwa mbona kwenye video inaonekana sura ya Chidi Benz akasema..."Ndio hapo sasa hiyo ni session nyingine... sasa nianze kuelekeza unataka kunirudisha Darasani?" akauliza Black X huku akicheka.
Hata hivyo, Director X amemshukuru Chid Benz kwa ushirikiano aliompatia hadi kukamilisha kazi hiyo na amewashukuru mashabiki zake na watu wote wanaomuunga mkono huku akiahidi kufanya kazi nyingi nzuri zaidi.
Director X alianza kujulikana baada kufanya video ya wimbo ‘Pombe na Muziki’ ya Byser (Mr Blue).
Kwa undani zaidi fuatilia mahojiano haya kupitia PMTV, Bofya hapa chini