Kwishaaaaa.! Chama wa Yanga kama wa Simba.
Joyce Shedrack
July 15, 2024
Share :
Farid Mussa amemkabidhi Clatous Chama jezi namba 17 iliyomtambulisha zaidi alipokuwa akiitumikia klabu ya Simba.
Kiungo huyo ambaye amehudumu ndani ya klabu Simba kwa misimu takriban 6 akiwa anavaa jezi namba 17 wakati anajiunga na wananchi alikuta jezi hiyo tayari inavaliwa na Farid Mussa na yeye kuanza kufanya mazoezi na jezi namba 20 ambayo hapo awali ilikuwa inavaliwa Zawadi Mauya.
Kupitia picha na video zilizochapishwa na klabu ya wananchi hii leo zimemuonesha Farid Mussa akiwa anamkabidhi mwamba wa Lusaka jezi yake pendwa yenye namba 17 mgongoni.
Kwa sasa Farid Mussa atakuwa anatambulika kwa jezi namba 12.