Kylie Jenner ashtua dunia kwa kuvaa sidiria ya shilingi Bilioni 132
Eric Buyanza
October 20, 2026
Share :

Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu duniani, Kylie Jenner, ameweka rekodi mpya ya kihistoria baada ya kuibuka kwenye jukwaa la mitindo la Victoria's Secret Fashion Show akiwa amevalia sidiria ya kifahari ya "Fantasy Bra" yenye thamani ya dola milioni 50 za Kimarekani (takriban shilingi bilioni 132 za Kitanzania).
Onyesho hilo lililofanyika tarehe 18 Oktoba 2026 jijini Los Angeles, limezua gumzo kubwa mitandaoni kutokana na thamani ya vazi hilo pamoja na uamuzi wa kampuni hiyo kumtumia Kylie Jenner kama mwanamitindo wao mkuu.
Sidiria hiyo iliyotengenezwa na kampuni maarufu ya vito vya kifahari ya Jacob & Co., sasa ndilo vazi la ndani ghali zaidi kuwahi kuonyeshwa katika historia ya miaka 30 ya Victoria's Secret. Vazi hilo limevunja rekodi ya awali ya dola milioni 15 iliyowekwa na mwanamitindo Gisele Bündchen mnamo mwaka 2000.
Sidiria hiyo imesukwa kwa dhahabu na kupambwa kwa almasi za asili 4,410.
Katikati ya vazi hilo kuna almasi kubwa ya njano yenye uzito wa karat 75.54, ambayo peke yake ina thamani ya dola milioni 22 (shilingi bilioni 58 za Kitanzania).





