LAMINE ACHAFUKWA: Sipendi kuangalia mechi za Bayern Munich, zinatabirika!
Eric Buyanza
September 19, 2026
Share :

Winga machachari wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Uhispania, Lamine Yamal, amezua gumzo kubwa kwenye ulimwengu wa soka kufuatia kauli yake kuwa hapendi kabisa kutazama mechi za miamba ya Ujerumani, Bayern Munich, kwa madai kuwa michezo yao haina msisimko kwa sababu huwa wanatawala kupitiliza.
Yamal alitoa kauli hiyo Ijumaa, Septemba 18, 2026 wakati akifanya mahojiano maalum na kituo cha habari cha Movistar Plus. Alipoulizwa kama huwa anafuatilia mechi za klabu kubwa barani Ulaya kupitia runinga, nyota huyo alikiri kutazama mechi za Real Madrid na PSG, lakini akaitosa Bayern Munich.
"Kusema ukweli, sipendi kabisa kuangalia mechi za Bayern. Kwa sababu kwenye ligi yao (Bundesliga), tayari najua kuwa watatawala sana mchezo kila wakati. Hata kwenye hatua ya makundi ya Champions League siangalii mechi zao kwa sababu wanazidominate sana timu pinzani," alisema Yamal.
Hata hivyo, kijana huyo alifafanua kuwa huwa anaangalia mechi za timu hiyo pale tu inapokutana na wapinzani wagumu:
"Ile mechi yao dhidi ya PSG ilikuwa nzuri sana, lakini kwenye hatua ya makundi sipendi kuwaangalia."





