pmbet

Lamine apona jeraha, atua kambini kuivaa England kesho

Eric Buyanza

November 14, 2026
Share :

Nyota chipukizi wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Lamine Yamal, amepona jeraha la goti na amejiunga rasmi na kikosi cha timu ya taifa tayari kwa mchezo mkali wa michuano ya UEFA Nations League dhidi ya England utakaopigwa kesho, Jumapili, Novemba 15, 2026.

 

Yamal, mwenye umri wa miaka 19, aliwasili katika kambi ya mazoezi ya timu hiyo iliyopo Las Rozas jijini Madrid, baada ya kusalia jijini Barcelona kwa siku kadhaa akipatiwa matibabu na kufanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madaktari wa klabu yake.

 

Winga huyo alilazimika kukosa mchezo uliopita siku ya Alhamisi ambapo Hispania iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech, kufuatia maumivu madogo ya goti aliyoyapata wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) dhidi ya Atlético Madrid.

 

Akizungumza na waandishi wa habari kuelekea pambano la kesho, Kocha Mkuu wa Hispania, Luis de la Fuente, amethibitisha kuwa nyota huyo yuko fiti kwa asilimia mia moja na yuko tayari kuikabili England.

 

Kurejea kwa Yamal ni habari njema kwa mashabiki wa Hispania kuelekea mchezo huo wa kukata na shoka dhidi ya England utakaochezwa kesho kuanzia saa 4:45 usiku, mchezo ambao utaamua kinara wa kundi lao katika michuano hiyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet