Lamine avunja rekodi hii ya Pele
Sisti Herman
July 10, 2024
Share :
Baada ya kuifunga goli moja kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Ufaransa kwenye nusu fainali ya kombe la Mataifa Ulaya (Euro 2024) Kiungo mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Hispania Lamine Yamal sasa amekuwa mfungaji mwenye umri mdogo zaidi kwenye michuano mikubwa ya kimataifa akivunja rekodi ilikuwa ikishikiliwa na mfalme wa soka Edson Arantes do Nascimento "Pele".
Lamine amefunga goli lake hilo la kwanza kwenye michuano ya EURO akiwa na miaka 16 na siku 362 huku rekodi ya awali ya Pele ikiwa ile aliyoweka kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 1958 dhidi ya Wales alipofunga goli akiwa na umri wa miaka 17 na siku 239.
Goli hilo la Lamine Yamal limewapeleka Hispania Fainali ambapo sasa wanasubiri mshindi kati ya Uingereza dhidi ya Uholanzi atakaye ungana nao fainali.