"Lamine ni mchezaji bora lakini sitamsajili"-Mourinho.
Joyce Shedrack
August 20, 2026
Share :
Kocha wa Real Madrid José Mourinho amemmwagia sifa nyota wa Barcelona Lamine Yamal kwa uwezo wake mkubwa, lakini ameweka wazi kuwa hana mpango wa kumsajili kinda huyo.

Mourinho alikiri kwamba Yamal ni mchezaji mwenye kiwango cha juu na mmoja wa vipaji vinavyong'ara zaidi katika soka la dunia kwa sasa huku akiweka wazi kuwa hakuna uwezekano wa kumsajili.
“Sitamsajili. Tayari tuna wachezaji bora.”
Yamal, ambaye amejijengea jina kubwa akiwa na Barcelona licha ya umri wake mdogo, amekuwa akivutia macho ya mashabiki na wadau wa soka kutokana na uwezo wake wa kiufundi, ubunifu na kiwango anachoonyesha uwanjani.
Hata hivyo Mourinho anaamini Real Madrid tayari ina wachezaji wenye uwezo wa kushindana na kufikia malengo makubwa zaidi bila kuhitaji huduma ya nyota huyo wa Barcelona.





