Lamine Yamal afikisha mechi 100 akiwa na umri wa miaka 17.
Joyce Shedrack
February 18, 2025
Share :
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Lamine Yamal ameweka rekodi ya kufikisha michezo 100 tangu aanze kucheza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 17.
Lamine ameifikia rekodi hiyo usiku wa jana baada ya kucheza mechi ya ligi kuu kati ya Barcelona na Rayo Vallecano ilipoibuka na ushindi wa goli 1-0.
Nyota huyo amefanikiwa kucheza mechi themanini na tatu (83) akiwa na Barcelona na mechi kumi na saba (17) akiwa na timu ya Taifa ya Hispania huku akifanikiwa kufunga magoli 21 na kutoa pasi za magoli 28 tangu acheze mechi yake ya kwanza mwezi Aprili mwaka 2023.