Lamine Yamal atengeneza cheni ya Bilioni 1 yenye aina yake ya ushangiliaji.
Joyce Shedrack
June 5, 2026
Share :
Nyota wa Timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Lamine Yamal amezua gumzo baada ya kununua cheni ya kipekee (custom chain) iliyotengenezwa kwa madini ya dhahabu huku ikikadiriwa kuwa na thamani ya Dola 400,000 ambazo ni zaidi ya Bilioni 1 za Kitanzania.
Jambo linavutia zaidi ni muundo wa cheni hiyo ambao ni mtindo wake maarufu wa ushangiliaji wa ‘304’ Namba hiyo inawakilisha namba za utambulisho wa posta (postal code) za mtaa wa Rocafonda huko Mataró, Catalonia, ambako ndiko alikozaliwa na kulelewa nyota huyo.





