pmbet

Lamine Yamal atuma ujumbe kuelekea fainali ya Kombe la Dunia.

Joyce Shedrack

July 15, 2026
Share :

Kinda nyota wa Hispania, Lamine Yamal, ameanza kuelekeza macho yake kwenye fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 baada ya kuisaidia Hispania kuichapa Ufaransa mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali.

Spain 'took a gamble' with Lamine Yamal as Barcelona star 'played more than  he should' on return from injury - Yahoo Sports

Mara baada ya Hispania kufuzu kucheza fainali yake ya pili katika historia ya Kombe la Dunia, Yamal alichapisha picha za mchezo huo kwenye ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na ujumbe uliosomeka: "Nueva York, vamos por ti," wenye maana ya "New York, tunakuja kwa ajili yako.”

 

Ujumbe huo unaonesha dhamira na ari ya kikosi cha Hispania kuelekea mchezo wa fainali utakaopigwa jijini New York, ambapo kitakuwa kikisaka kutwaa taji la pili la Dunia.

 

Yamal mwenye umri wa miaka 19, alikuwa mmoja wa vijana wawili waliopangwa kwenye kikosi cha kwanza cha La Roja, sambamba na Pau Cubarsí, jambo lililoweka rekodi mpya katika historia ya Kombe la Dunia la FIFA.

 

Hii ilikuwa mara ya kwanza kabisa kwa timu moja kuanza mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Dunia ikiwa na wachezaji wawili wenye umri wa chini ya miaka 20 kwenye kikosi cha kwanza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet