Lamine Yamal awabwaga kinda wa Madrid tuzo ya Laliga.
Joyce Shedrack
June 5, 2025
Share :
Mshambuliaji wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania Lamine Yamal amechaguliwa kuwa mchezaji bora chini ya umri wa miaka 23 wa ligi kuu ya Hispania laliga.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 17 ambaye hivi karibuni ameongoza mkataba wa kusalia ndani ya Barcelona ameshinda tuzo hiyo baada ya kuonesha kiwango bora msimu uliopita.
Lamine amecheza mechi 35 za ligi akifunga jumla ya magoli 9 na kutoa pasi 13 za magoli akiisadia klabu yake kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa msimu uliotamatika wa 2025/25.