Lamine Yamal aweka rekodi mpya Barcelona.
Joyce Shedrack
July 17, 2025
Share :
Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona Lamine Yamal ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuvaa jezi namba 10 akiitumikia klabu hiyo.

Yamal ambaye ameongeza mkataba mpya na Barcelona hadi mwaka 2031 siku ya leo kwa mara ya kwanza ametambulishwa rasmi akiwa amevaa jezi ya namba 10 ambayo itakuwa utambulisho wake uwanjani kuanzia msimu ujao.
Nyota huyo aliyetimiza miaka miaka 18 siku chache zilizopita anakuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuvaa jezi hiyo akivunja rekodi ya Ansu Fati aliyekuwa na miaka 19 alipokabidhiwa namba hiyo baada ya kuondoka kwa Lionel Messi mwaka 2021.
Jezi namba 10 ya Barcelona imewahi kuvaliwa na wachezaji wakubwa kama Lionel Messi, Ronaldinho, Rivaldo na Stoichkov.