pmbet

Lamine Yamal na jeuri ya jumba lenye thamani ya Bilioni 34 za kibongo

Eric Buyanza

July 30, 2026
Share :

Nyota wa klabu ya Barcelona, Lamine Yamal anamiliki jumba la kifahari lenye thamani inayokadiriwa kufikia Euro milioni 11 (sawa na takriban shilingi bilioni 34 za Kitanzania ambalo lipo kwenye eneo la kifahari linaloitwa 'Ciutat Diagonal' linalokaliwa na mabilionea jijini Barcelona.

 

Jumba hili lina historia maarufu kwani zamani ilikuwa ikimilikiwa na beki wa zamani wa Barcelona, Gerard Piqué, pamoja na aliyekuwa mkewe mwanamuziki mashuhuri Shakira.

 

SIFA ZA NYUMBA

Ina ukubwa wa eneo la mita za mraba 3,800 likiwa na majengo matatu tofauti, vyumba sita vikubwa vya kulala, kiwanja kidogo cha mpira wa miguu, studio ya kurekodia muziki (iliyotumiwa na Shakira zamani), bila kusahau chumba cha kuangalizia sinema, bwawa kubwa la kuogelea na Gym ya kufanyia mazoezi.

 

Kabla ya kununua jumba hili kwa ajili yake mwenyewe, Yamal alikuwa tayari ameshanunua nyumba tatu tofauti kwa ajili ya mama yake, baba yake pamoja na bibi yake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet