Laporta amtuhumu Xavi kutumika na mpinzani wake.
Joyce Shedrack
March 9, 2026
Share :
Mgombea urais wa FC Barcelona, Joan Laporta, amemtuhumu kocha wa zamani wa klabu hiyo Xavi Hernández kutumika na mpinzani wake anayegombea pia nafasi hiyo ya Urais.
Laporta amemlaumu Xavi kwa kukubali kutumika baada ya kauli alizozingumza katika mahojiano yake aliyoyafanya siku ya jana akidai kuwa mshirika wa karibu wa Laporta, Alejandro Echevarria, ndiye anayeendesha mambo ndani ya klabu.

“Inaniuma kwamba alijiruhusu kutumiwa na kwamba alimshambulia Alejandro Echevarria ili kuniumiza. Echevarría na Rafael Yuste walitetea kubaki kwa Xavi hadi mwisho,”
“Nyuma ya Xavi kuna mtu anayemtumia, na huyo ni Víctor Font. Anajaribu kuchafua mambo. Malalamiko kutoka kwa mwanachama pia yalifanya kazi kwa manufaa yake, yakampa uaminifu.”





