Lavalava alia kufanyiwa fitna kwenye kazi zake.
Joyce Shedrack
August 20, 2025
Share :
Staa wa muziki wa bongofleva Lava Lava amefunguka kuhusu changamoto anazokabiliana nazo kwenye muziki huku akianika ukweli kuwa yeye ndiye msanii wa kwanza anyeoongoza kwa kufanyiwa fitina kwenye kazi zake.
Lava Lava ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa instagram akisema mara zote anafanyiwa fitina pale tu anapotangaza kutoa muziki mpya.
“Mpaka sasa mimi ndiye msanii ninayeongoza kwa kufanyiwa fitina kila ninapotoa kazi mpya ila Mungu yupo na mimi” Ameandika Lava lava.