pmbet

Lazima Medeama walipie kwa hili! - Ali Kamwe

Eric Buyanza

December 4, 2023
Share :

Afisa habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ally Shaban Kamwe amekiri kuwa wamezianza vibaya hesabu za kukusanya alama kwenye hatua ya makundi ya ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwenye michezo miwili ya mwanzo na kusisitiza kuwa lazima wakatafute ushindi ungenini dhidi ya Medeama ili kufidia alama walizoangusha.
 

"Tumepoteza ugenini na kutoa sare nyumbani, tumepata alama 1 kati 6 tuzohitaji kwa Al Ahly na Belouizdad, matumaini yetu yapo kwa Medeama, twende tukafe naye Ghana, tufe naye hapa tukiweza kupata alama 6 kwao mechi nyingine ya nyumbani itakuwa dhidi ya Belouizdad ambayo itatupeleka robo fainali" alisema Kamwe.
 

Yanga imeambulia alama moja pekee kwenye michezo miwili ya mwanzo ya hatua hiyo waliyopigania kuwepo kwa zaidi ya miaka 25 sasa wanatafuta robo fainali wakiburuza mkiwa kwenye kundi D.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet