Lazima nirudi shule, kule ndiko kwenye mipango - Chino
Eric Buyanza
May 17, 2025
Share :
Msanii wa Bongo Fleva, Chino Kidd amesema pamoja na umaarufu wake anahitaji sana kurudi shule ili aongeze uwezo wake wa kuimba.
"Mimi shule lazima nirudi tu, kwani kule ndo kwenye mipango na maisha mazuri, naelewa bila shule mambo mengi tunakuwa tunafanya lakini tunakosea, mashabiki wangu ambao wanatamani kuniona nikirudi shule wanaamini nitafanya hivyo kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kazi yangu," alisema Chino.
"Sasa hivi nimeshaanza kuifahamu lugha ya Kiingereza, natamani sana kuifahamu kuongea zaidi, mpenzi wangu mzungu anajitihida kubwa sana kunifundisha, japo watu wameanza kuzusha nimeachana nae.
Mimi ni mwehu niachane na mwalimu wangu wa lugha? bado nipo naye na ninatamba naye," alisema Chino.
MWANASPOTI