Lazima utoe jasho na upigane kuwashinda Arsenal - Guardiola
Eric Buyanza
April 22, 2026
Share :

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amewamwagia sifa Arsenal kabla ya safari yake ya kwenda Burnley usiku wa leo.
City watakuwa na nafasi ya kuwashusha kileleni Arsenal ikiwa watashinda mchezo wao wa leo dhidi ya Burnley.
Guardiola, ambaye timu yake iliishinda Arsenal 2-1 siku ya Jumapili, bado amesema wapinzani wao wa ubingwa ni miongoni mwa timu bora barani Ulaya.
“Arsenal ni timu ya viwango vya juu na lazima utoe jasho na upigane sana kuwashinda kwa kuwa wana kila kitu” alisema Guardiola.
Kwa mujibu wa kocha huyo wachezaji wa Arsenal wanapambana sana na wana mambo mengi mazuri.....kwa mfano pasi fupi, ndefu na mipira ya juu wanacheza vizuri bila kusahau mipira ya kutenga (set pieces).





