LeBron James na Will Smith watembelea Angola
Sisti Herman
September 13, 2026
Share :

Rais wa Angola, João Lourenço, aliwapa LeBron James na Will Smith jezi maalum za timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Angola wakati wa ziara yao jijini Luanda.
Mastaa hao wawili kutoka Marekani walikaribishwa na rais wakati Angola ikiandaa mashindano ya boti za kasi za umeme ya E1 katika mji mkuu huo.
Timu ya LeBron, Team AlUla, na timu ya Will Smith, Westbrook Racing, ni miongoni mwa timu zinazoshiriki mashindano hayo yaliyowaleta mastaa hao wa kimataifa katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.





