pmbet

LEGEND...! Samatta aweka rekodi nyingine Ulaya

Sisti Herman

April 12, 2024
Share :

Mara baada ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na KRC Genk ya Ubelgiji, ligi ya Uefa Europa league akiwa na Royal Anterp FC sasa Mshambuliaji na Nahodha wa Tanzania Mbwana Ally Samatta ameendeleza rekodi kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza michuano yote mikubwa ya Ulaya ambayo ameikamilisha msimuu kwa kucheza Uefa Conference league akiwa na PAOK Thesalonike ya Ugiriki ambayo jana ilipoteza 1-0 kwa Clubb Brugge kwenye robo fainali.

Rekodi hiyo ya Samatta inaenda sambamba na namba nzuri ambapo kati ya michezo 19 ya michuano ya Ulaya aliyocheza amefunga mabao 7 ukiwa ni wastani bora kwa mchezaji kutoka Afrika, ambapo;

- Uefa Champions league amecheza mechi 6 na kufunga goli 3,
- Uefa Europa League amecheza mechi 6 na kufunga goli 3,
- Uefa Conference League amecheza mechi 7 na kufunga goli 1.

Samatta ndiyo mwanasoka Mtanzania aliyefanikiwa zaidi kucheza hatua kubwa hadi sasa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet