pmbet

Leicester warejea ligi kuu Uingereza

Sisti Herman

April 27, 2024
Share :

Baada ya Leeds United kupoteza jana kwa 4-0 kutoka kwa QPR kwenye ligi daraja la kwanza nchini Uingereza (Championship), klabu ya Leicester City sasa wamepanda daraja rasmi na sasa wamerejea kwenye ligi kuu Uingereza.

Leicester wamepanda daraja moja kwa moja wakiwa juu kwenye msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 94 ambazo haziwezi kufikiwa na timu inayoshika nafasi ya pili, Leeds ambao wamesalia kuwa na alama 90 huku ikiwa imebakiwa na mchezo mmoja tu tofauti na Leicester iliyosaliwa na michezo miwili kwenye ligi hiyo yenye timu 24.

Leicester waliwahi kuwa mabingwa ligi kuu Uingereza msimu wa 2015/16.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet